Na mwandishi wetu
Mwamuzi Elly Sasii wa Dar es Salaam ndiye atakayesimama katikati kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu ya soka Tanzania, Yanga na Simba itakayopigwa Agosti 8, 2024 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo maarufu Kariakoo/Dar Derby, mwamuzi huyo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga pamoja na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam wakati Amin Kyando wa Morogoro atakuwa mwamuzi wa akiba.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumanne hii pia ilimtaja, Soud Abdi kutoka mkoani Arusha kubeba jukumu la kuwa mtathmini wa waamuzi wa mechi hiyo.
Viingilio vya mechi hiyo ni Sh 50,000 kwa VIP A, Sh 30,000 (VIP B), Sh 20,000 (VIP C), Sh 10,000 (Machungwa) na Sh 5,000 (Mzunguko).
Katika mechi nyingine ya Ngao ya Jamii siku hiyo hiyo, Azam itaumana na Coastal Union kwenye dimba la Amaan Complex ambapo Ahmed Arajiga wa Manyara atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Janeth Balama wa Iringa na Ally Ramadhan wa Zanzibar.
Mwamuzi wa akiba katika mechi hiyo atakuwa ni Nasrah Siyah wa Zanzibar wakati mthamini wa waamuzi hao atakuwa ni Victor Mwandike wa Mtwara wakati viingilio vya mechi hiyo vinaanzia Sh 5,000, Sh 3,000 na Sh 2,000.
Washindi wa mechi hizo ambazo ni za nusu fainali wataumana katika mechi ya fainali ambayo itatoa bingwa wa Ngao ya Jamii, michuano ambayo huashiria ufunguzi wa msimu mpya wa ligi ya soka nchini Tanzania.
Soka Sasii akabidhiwa Dar Derby
Sasii akabidhiwa Dar Derby
Read also