Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane ataikosa mechi ya timu hiyo ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024-25 dhidi ya timu yake ya zamani ya Tottenham Hotspur itakayopigwa mjini Seoul, Korea Kusini.
Kane alijiunga na Bayern majira ya kiangazi msimu uliopita akitokea Spurs kwa ada ya dola 130 milioni na kumaliza msimu wa kwanza akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga kwa kufunga mabao 36.
Mabao hayo ya Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya England hayakuiwezesha Bayern kubeba taji la Bundesliga badala yake timu hiyo iliishia nafasi ya tatu ikizidiwa pointi 18 na vinara wa ligi hiyo, Bayer Leverkusen.
Kane aliumia mgongo kabla ya kuiwakilisha England kwenye fainali za Euro 2024 nchini Ujerumani na aliifungia timu hiyo mabao matatu na kuifikisha hatua ya fainali ya michuano hiyo.
England hata hivyo ilishindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji hilo wakati Kane hakuwa katika ubora wake uliozoeleka hali iliyomfanya akosolewe mara kwa mara na wachambuzi wa soka.
Bayern katika maandalizi ya msimu mpya inaweka kambi Korea Kusini ambapo itapata nafasi ya kujipima nguvu dhidi ya Spurs, timu ambayo Kane aliichezea kwa mafanikio na anashikilia rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao mengi (280).
“Harry Kane, Kingsley Coman, Dayot Upamecano na Alphonso Davies hawatakuwapo ingawa natumaini watakuwa fiti kwenye mechi ya kikombe,” alisema kocha wa Bayern, Vincent Kompany.
Kimataifa Kane kuikosa mechi ya Bayern, Spurs
Kane kuikosa mechi ya Bayern, Spurs
Read also