Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kulia, Kelvin Kijili *(pichani) kutoka Singida Fountain Gate kwa mkataba wa miaka miwili.
Ujio wa Kijili aliyetangazwa Ijumaa hii na Simba au Wekundu wa Msimbazi kupitia mitandao yao ya kijamii anakuja kusaidiana na mkongwe Shomari Kapombe kwenye nafasi ya beki wa kulia.
Kijili, 24 tayari ameripotiwa kujiunga na wenzake kambini nchini Misri kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2024-25.
“Akiwa na Singida Fountain Gate msimu uliopita Kijili amesaidia kupatikana kwa mabao manne (assisti).
“Kijili amekuja kuongeza kitu kikubwa kwenye kikosi chetu na kutokana na umri alionao tunaamini ataendelea kuwa msaada kwa timu kwa muda mrefu,” ilieleza sehemu ya taarifa ya Simba.
Wekundu hao wamefafanua kuwa usajili waliofanya kuelekea msimu mpya wa mashindano wamezingatia kigezo cha umri kwa kuwa malengo yao ni kujenga timu imara ya muda mrefu.
Soka Kijili amwaga wino Msimbazi
Kijili amwaga wino Msimbazi
Related posts
Read also