Berlin, Ujerumani
Timu za taifa za Ujerumani na Marekani zinadaiwa kuanza mbio za kutaka kumuajiri kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp.
Ujerumani mwenyeji wa fainali za Euro 2024, tayari imetolewa katika fainali hizo na Klopp ambaye wamekuwa wakimuwinda kwa muda mrefu sasa ni wakati sahihi kwake kuchukua nafasi ya kocha Julian Nagelsmann.
Klopp ambaye ni Mjerumani aliamua kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu ulioisha hivi karibuni wa 2023-24, hadi sasa hajasema lolote kuhusu timu atakayojiunga nayo baada ya Liverpool.
Baada ya kuondoka Liverpool matarajio ya wengi ni kwamba kocha huyo alikuwa akielekea kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani kabla ya timu hiyo kumpa majukumu hayo Vincent Kompany.
Kwa upande wa Marekani, timu hiyo pia mambo yake si mazuri kwenye fainali za Copa America ambazo zinaendelea nchini humo na inaamini Klopp anafaa kuchukua nafasi ya Gregg Berhalter.
Kimataifa Klopp atakiwa Ujerumani, Marekani
Klopp atakiwa Ujerumani, Marekani
Read also