Na mwandishi wetu
Hatimaye kiungo fundi Mzambia, Clatous Chama amevunja ukimya na kuwashukuru Simba katika muda wote aliokaa nao mpaka alipotangazwa kuibukia kwa mahasimu wao Yanga.
Chama ameeleza hisia zake hizo akiwaaga Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii leo Jumatano huku akiwashukuru kwa muda wote wa miaka sita waliodumu na kuandika historia pamoja.
“Wapendwa familia ya Simba, miaka sita iliyopita nilikuja kwenu kama mgeni. Mlinipa kusudi na changamoto ya kuwa toleo bora zaidi ya nilivyokuwa.
“Tuliteka ardhi hii pamoja, tukapanua utawala wetu hadi sehemu nyingine za Afrika, na kilichobaki ni historia.
“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na kusudi, hatima zetu zilizounganishwa huchukua uelekeo tofauti, sina chochote ila heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na msaada mlionipa miaka yote hii, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha historia tuliyotengeneza pamoja,” ilifafanua sehemu ya ujumbe huo.
Hata hivyo, Chama ambaye tangu atangazwe kutua Yanga juzi alikuwa hajabadili wasifu wake kwenye mitandao ya kijamii, sasa ameelekeza yeye ni mchezaji wa Yanga na si Simba kama ilivyokuwa ikisomeka awali.
Soka Chama aaga rasmi Simba
Chama aaga rasmi Simba
Read also