Na mwandishi wetu
Siku kadhaa baada ya Coastal Union kutangaza kuachana na beki wake, Felly Mulumba, (pichani) uongozi umefunguka kuwa kikwazo ni umri wa beki huyo.
Akizungumza hivi karibuni na GreenSports, Ofisa Habari wa Coastal, Abbas El Sabri alisema mashabiki wa Wagosi Wakaya hao hawapaswi kuvunjika moyo kwa kuondoka kwa Mulumba kwani huo ni mchakato wa kuisuka Coastal bora zaidi.
“Hapana tatizo katika hilo, inafahamika Mulumba ni beki mkubwa, muhimu na alikuwa nguzo ya kutuliza timu lakini kwa kuangalia umri wake tumeona anahitaji kwamba tutafute vijana ambao wataleta nguvu na changamoto mpya,” alisema El Sabri.
Alieleza kuwa kwa sasa wanatengeneza kikosi ambacho kitadumu kwenye michuano ya kimataifa kwa takriban misimu mitatu baada ya msimu huu kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Coastal mbali na Mulumba, 36, pia imeondokewa na beki wake mwingine, Lameck Lawi, 18 aliyetangazwa kujiunga na Simba SC huku ikielezwa tayari kuna beki kisiki kutoka Uganda yupo kwenye mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo ya mjini Tanga ili kuendeleza moto msimu ujao.
Soka Coastal yataja sababu kumuacha Mulumba
Coastal yataja sababu kumuacha Mulumba
Read also