Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imetangaza kuachana na beki wake wa kati, Henock Inonga Bacca baada ya kuitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo.
Taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo iliweka wazi uamuzi huo na kumtakia kila la heri beki huyo ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya DR Congo.
Inonga anakuwa mchezaji mwingine kuachwa na uongozi wa Simba katika siku za hivi karibuni baada ya kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye ni raia wa Burundi.
Inonga atakumbukwa kwa namna ambavyo ametoa mchango mkubwa kwa timu hiyo hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali mara tatu.
Uamuzi huo ni katika mikakati ya uongozi wa Simba kukisuka upya kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa 2024-25 baada ya kutoridhishwa kwa ujumla na mwenendo wa timu yao katika msimu wa 2023-24.
Simba imemaliza msimu wa 2023-24 ikiwa nafasi ya tatu katika Ligi Kuu NBC pamoja na kufikia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa inajiandaa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao wa 2024-25.
Soka Inonga naye aachwa Simba
Inonga naye aachwa Simba
Read also