Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said amempokea mgeni wake beki wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Morocco, Achraf Hakimi leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Hakimi ambaye ni mchezaji bora wa PSG msimu wa 2023-24, ameelezwa kwamba atadumu Tanzania kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
Awali, Hersi alikutana na Hakimi nchini Ufaransa, Januari 3, mwaka huu baada ya kupata mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Klabu ya PSG l, Nasser Al-Khelaifi.
Imefafanuliwa kuwa baada ya kukutana na Hakimi, Hersi alitumia nafasi hiyo kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Inter Milan na Borussia Dortmund kutembelea vivutio mbalimbali vya Tanzania.
Na sasa ushawishi huo umelipa, Hakimi ametua nchini akiwa na rafiki zake saba kwa ajili ya kufanya utalii huo.
Kimataifa Hersi ampokea Hakimi Tanzania
Hersi ampokea Hakimi Tanzania
Read also