Na mwandishi wetu
Beki wa kati, Lameck Lawi (pichani akiwa na Juma Mgunda) amekuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Simba SC kwenye usajili wa timu hiyo kuelekea msimu ujao wa 2024-25.
Utambulisho wa Lawi ni kama umekuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na beki mwingine wa kati mzawa Kennedy Juma waliyetangaza kuachana naye Alhamisi hii mchana.
Beki huyo, 18 amepewa mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi baada ya msimu uliopita kuonesha kiwango cha kuvutia akiwa na Coastal Union.
Katika Ligi Kuu NBC msimu wa 2023-24 uliomalizika hivi karibuni, Coastal imemaliza ligi hiyo ikiwa nafasi ya nne na kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Simba, imeeleza kuhusu usajili huo kwa kuandika: “Lawi ni kijana mwenye kipaji kikubwa na amekuwa ngome imara kwenye kikosi cha Coastal msimu uliopita na hicho ndicho kilichotuvutia kumsajili.
“Usajili wa Lawi ni mkakati wa kuijenga Simba mpya yenye ushindani kuelekea msimu wa mashindano wa 2024-25 na usajili wake tunategemea utaongeza kitu kikubwa katika kikosi akisaidiana na walinzi wazoefu waliokuwepo.”
Soka Lameck Lawi atua Simba
Lameck Lawi atua Simba
Read also