Na mwandishi wetu
Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, Ismael Aden Rage amejitokeza na kueleza furaha yake baada ya Tabora United kubaki Ligi Kuu NBC, akiahidi sasa ni wakati wa timu hiyo kupata udhamini wa kishindo na kutikisa kwenye ligi hiyo.
Rage amesema kuanzia msimu ujao Tabora itapata udhamini mzuri akidai kuwa ni mapema kuweka wazi vitu vingi lakini binafsi ameshamaliza kazi yake sasa ni zamu ya uongozi wa Tabora United.
“Kama mwenyeji wa Tabora nataka niwape ahadi kwamba kuanzia msimu unaokuja (Tabora) watapata mdhamini wa kishindo kiasi kwamba wasipate taabu ya kuwa ombaomba tena.
“Ni mapema sana kusema lakini nawaachia viongozi wao wasaini mkataba, mimi nimeshamaliza kazi, sababu sasa timu itakwenda kubadilika kuanzia usajili na mengine baada ya kushauriana na wadau kuungana kwa pamoja,” alisema Rage mwenyekiti wa zamani wa Simba SC.
Rage ambaye pia amewahi kuwa katbu mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa TFF alisema: “Ni furaha kubwa, kwa sababu Mkoa wa Tabora una histotia kubwa ya kisiasa na michezo, wachezaji wengi mabingwa wametoka Tabora kwa hiyo ingekuwa aibu Tabora kuingia na kushuka mwaka huo huo. Jitihada imefanywa kubwa na wachezaji na mashabiki na kupata ushindi.”
Tabora imefanikiwa kusalia Ligi Kuu NBC baada ya jana Jumapili kuifunga timu ya Biashara Mara mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na kuondoka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Soka Tabora Utd wamkosha Rage
Tabora Utd wamkosha Rage
Read also