Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la usajili kuelekea msimu ujao wa 2024-25, ambapo litafunguliwa Juni 15 Jumamosi hii na kufungwa Agosti 15, mwaka huu.
Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa hii na shirikisho hilo imefafanua kuwa dirisha hilo ni kwa ajili ya Ligi Kuu NBC, Ligi ya Championship, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Kuu ya Wanawake.
TFF pia imesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada wa usajili baada ya kufungwa kwa dirisha hilo, hivyo imezitaka klabu zote kuzingatia muda huo.
Na pia katika taarifa hiyo, shirikisho hilo limeweka wazi kuwa dirisha dogo la usajili msimu ujao litakuwa wazi kuanzia Desemba 16, mwaka huu na kufikia ukingoni Januari 15, mwakani.
Wakati TFF ikitoa taarifa hiyo tayari klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zimeanza kuhusishwa na wachezaji kadhaa wa kuwasajili wakiwamo wa kuwaaacha.
Soka TFF yatangaza kuanza kwa usajili
TFF yatangaza kuanza kwa usajili
Read also