Ndola, Zambia
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka shujaa ugenini baada ya kuigonga Zambia maarufu Chipolopolo kwa bao 1-0 katika mechi ya Kundi E ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumanne hii jioni kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Stars iliandika bao hilo mapema dakika ya tano mfungaji akiwa ni Waziri Junior.
Zambia licha ya kuwa uwanja wa nyumbani na kupambana kutaka kusawazisha lakini mambo yalikuwa magumu kwani hadi mwamuzi Abdelazid Bouh anapuliza filimbi ya kumaliza mchezo, matokeo yalibaki kuwa mazuri kwa Stars.
Kwa ushindi huo Stars sasa imefikisha pointi sita na kuwa katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo ambalo linaongozwa na Morocco waliofikisha pointi tisa baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Congo.
Katika kundi hilo Stars inafuatiwa na timu za Zambia na Niger zenye pointi tatu kila moja wakati Congo na Eritrea hazijavuna pointi hata moja hadi sasa.
Kimataifa Stars yaigonga Zambia 1-0
Stars yaigonga Zambia 1-0
Read also