Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki amefichua juu ya ujio wa mshambuliaji Mzimbabwe katika timu hiyo, Prince Dube aliyekuwa akiitumikia Azam FC.
Mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu NBC msimu wa 2023-24 amesikika akizungumza hayo alipokuwa akizungumza mubashara na meneja wa kitengo cha dijiti Yanga SC, Priva Abiudi kupitia mtandao wa Instagram na video yao kusambaa kwa kasi.
Katika video hiyo, Aziz anasikika akisema msimu ujao atahakikisha anawasaidia washambuliaji wa timu hiyo kutwaa kiatu cha ufungaji bora, miongoni mwa washambuliaji hao akiwataja ni Dube na kuonesha wazi kuwa straika huyo atavaa uzi wa Yanga msimu ujao.
“Dube anakuja, (Joseph) Guede yupo, nisikilize, mimi ni kiungo, nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanakuwa wafungaji bora. Mimi ni kiungo kwa nini niwanie ufungaji bora, kwa nini ununue straika halafu utake kiungo awe mfungaji bora?” Alihoji Aziz Ki raia wa Burkina Faso.
“Mimi ahadi yangu, nina matumaini straika wa Yanga atakuwa mfungaji bora msimu ujao Mungu akipenda, lakini sio Aziz, sahau kuhusu Aziz, mimi nitatoa asisti na siyo kuwa mfungaji bora,” alifafanua mchezaji huyo wa zamani wa Asec Mimosas.
Kauli hiyo ya Aziz Ki inaweza kuwa njema zaidi kwa Wanayanga ambao kwa muda mrefu wamekuwa na sintofahamu baada ya kuwepo kwa taarifa za kiungo huyo kuwa njiani kuondoka.
Taarifa hizo zinahusishwa zaidi na mkataba wa mchezaji huyo kumalizika lakini hapo hapo furaha zaidi ikiibuka baada ya kupata uhakika wa asilimia nyingi juu ya uhamisho wa Dube ambaye pia anawaniwa na Simba SC.
Soka Aziz Ki afichua ishu ya Dube Yanga
Aziz Ki afichua ishu ya Dube Yanga
Read also