Na mwandishi wetu
Wazari Mkuu, Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Yanga kwa kuandaa mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumapili hii.
Katika salamu hizo, kiongozi huyo wa serikali pia aliwapongeza, viongozi, wachezaji na wanachama kwa kuimarisha umoja na mshikamano kwa miaka mitatu mfululizo.
Waziri Mkuu pia aliwapongeza Yanga kwa kufanya vizuri zaidi mwaka huu na kusisitiza juu ya kuuhamasisha umma katika kupanga na kutekeleza mambo yao kwenye michezo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Katika pongezi hizo Waziri Mkuu pia aliwatakia heri Yanga kwa msimu ujao huku akisema kwamba anaamini wengine watajifunza kutoka Yanga na katika hilo akawataja watani wa Yanga ambao ni timu ya Simba.
Yanga wamefanya mkutano wao wa wanachama katika mazingira ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa bora na kwa weledi wa hali ya juu.
Kwa ujumla katika miaka ya karibuni mikutano ya wanachama wa Yanga imekuwa ikiendeshwa katika hali ya utulivu tofauti na ambavyo imekuwa ikijitokeza katika miaka ya nyuma.
Soka Waziri Mkuu awapongeza Yanga
Waziri Mkuu awapongeza Yanga
Read also