Manchester, England
Kocha wa Man United Erik ten Hag analazimika kusubiri kabla ya kujua hatma yake katika klabu hiyo kama atatimuliwa au ataendelea na kibarua chake kama kawaida.
Awali zilikuwapo habari kwamba kocha huyo angetimuliwa Mei 25 baada ya mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City lakini jambo hilo halikufanyika pengine kwa kuwa Man United iliibuka kinara na kubeba kombe hilo.
Habari zaidi zinadai kwamba vigogo wa klabu hiyo kupitia kampuni ya INEOS wameendelea na mchakato wa kufanya tathmini ya mwenendo wa timu hiyo tangu wapate ushindi wa FA kabla ya kuamua kuachana au kuendelea na Ten Hag.
Inadaiwa kwamba uamuzi wowote kuhusu hatma ya Ten Hag ndio msingi wa tathmini inayoendelea na huenda lolote linaweza kutangazwa wiki hii baada ya kushindikana Mei 25 kama ilivyodaiwa awali.
Ten Hag hadi sasa hajaambiwa lolote na mabosi wake na hakuna muda maalum uliotangazwa kuhusu hatma yake na kwa sasa ni kama vile ameendelea kubaki njia panda akisubiri uamuzi wowote utakaofikiwa.
Man United ingawa imebeba taji la FA baada ya kuinyuka Man City mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley, kitendo cha timu hiyo kumaliza nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu England (EPL) ndicho kinaacha maswali kuhusu hatma ya kocha huyo.
Kimataifa Ten Hag awekwa kiporo
Ten Hag awekwa kiporo
Read also