London, England
Kocha wa England, Gareth Southgate ameamua kutangaza kikosi cha timu hiyo cha wachezaji 26 mapema kwa ajili ya fainali za Euro 2024 ili kuwa katika utulivu na kuweka akili kwenye mechi yao ya leo Ijumaa dhidi ya Iceland.
Leo England inaumana na Iceland ambapo jana jioni Southgate alitangaza kikosi chake ikiwa ni siku moja kabla ya mechi hiyo ya mwisho ya kujipima nguvu kabla ya fainali za Euro 2024 zitakazoanza Juni 14.
Awali Southgate alitangaza kikosi cha wachezaji 33 lakini sasa ameamua kupunguza idadi hiyo kabla ya kuelekea kwenye fainali za Euro 2024 nchini Ujerumani.
“Sikutaka wachezaji wasubiri hadi Ijumaa hilo kwa hakika lingekuwa janga, isingekuwa sawa kwa wachezaji tuliowaacha na isingekuwa sawa kwa wachezaji kusubiri kuthibitishiwa kwamba wapo kwenye timu,” alisema Southgate.
Kikosi cha England na timu za wachezaji kwenye mabano ni kama ifuatavyo, makipa: Aaron Ramsdale (Arsenal), Dean Henderson (Crystal Palace) na Jordan Pickford (Everton).
Mabeki: Luke Shaw (Man United), John Stones (Man City), Kieran Trippier (Newcastle), Joe Gomez (Liverpool) Lewis Dunk (Brighton), Marc Guehi (Crystal Palace), Ezri Konsa (Aston Villa) na Kyle Walker (Man City).
Viungo: Kobbie Mainoo (Man United) Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Conor Gallagher (Chelsea), Adam Wharton (Crystal Palace) na Kobbie Mainoo (Man United) na Declan Rice (Arsenal).
Washambuliaji: Jude Bellingham (Real Madrid), Cole Palmer (Chelsea), Bukayo Saka (Arsenal), Jarrod Bowen (West Ham), Eberechi Eze (Crystal Palace), Phil Foden (Man City), Anthony Gordon (Newcastle), Harry Kane (Bayern Munich), Ivan Toney (Brentford) na Ollie Watkins (Aston Villa).
Walioachwa kutoka orodha ya awali ni Harry Maguire, James Trafford, Jack Grealish, James Maddison, Jarrad Branthwaite, Jarell Quansah na Curtis Jones.