Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Mei huku mshambuliaji wa Mashujaa FC, Reliant Lusajo akiteuliwa mchezaji bora, wote kwa msimu huu wa 2023-24 wa Ligi Kuu NBC.
Taarifa ya Idara ya habari, mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilimtaja Lusajo kuwa mshindi akiwabwaga, Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum au Fei Toto wa Azam FC.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kamati ya tuzo hizo ya TFF ilimteua Lusajo kwa kuwa alikuwa msaada mkubwa kwa timu yake katika ushindi wa mechi nne kati ya sita za timu hiyo kwa kipindi cha mwezi Mei.
Mchango wa Lusajo uliiwezesha Mashujaa kukusanya pointi 12 na hivyo kupanda kutoka nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC hadi nafasi ya nane huku Lusajo akifunga mabao matano na kuwa ‘mpishi’ wa mabao mengine mawili.
Kwa upande wa Mgunda ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya Abdelhak Benchikha kuamua kuachia ngazi, yeye ameiwezesha Simba katika kipindi hicho kushinda mechi zake dhidi ya Tabora United, Azam, Prisons, Geita, KMC, JKT na kutoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar.
Mgunda katika kinyang’anyiro cha kocha bora wa mwezi Mei alikuwa akishindana na Miguel Gamondi wa Yanga na Bruno Ferry wa Azam.
Kamati ya tuzo pia imemteua meneja wa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Juma Amir kuwa meneja bora wa mwezi Mei kutokana na usimamizi mzuri wa matukio ya uwanjani pamoja na masuala yanayohusu miundombinu ya uwanja
Soka Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei
Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei
Read also