Manchester, England
Klabu ya Man City inadaiwa kujiandaa kumsainisha mkataba mpya mshambuliaji, Erling Haaland ambaye ndio kwanza ana miaka 23 na tayari ameonesha ubora wake wa kuzifumania nyavu.
Mshambuliaji huyo kutoka Norway amewahi kuhusishwa na mipango ya kujiunga na klabu ya Real Madrid miaka ya nyuma lakini katika miezi ya karibuni habari hiyo ilianza kupoteza umaarufu.
Katika habari hiyo, ilikuwa ikielezwa kwamba katika mkataba wa Haaland na Man City kuna kipengele ambacho kinaipa nafasi Real Madrid kumsajili mshambuliaji huyo.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amewahi kuikanusha habari hiyo lakini bado mshambuliaji huyo aliendelea kuhusishwa na Real Madrid mara kwa mara hasa wakati wa usajili.
Kwa mujibu wa gazeti moja la Uingereza, kwa sasa Man City wamepania kuhakikisha wanamalizana na mshambuliaji huyo kwa kumpa mkataba mrefu.
Mpango huo wa Man City hata hivyo si kweli kwamba una uhakika wa asilimia 100 hasa kwa kuwa Haaland ni aina ya mshambuliaji ambaye anahitajika pia na klabu nyinginezo ukiacha Real Madrid.
Zipo habari kwamba PSG ya Ufaransa nayo inasaka mshambuliaji wa hadhi atakayechukua nafasi ya Kylian Mbappe ambaye anatajwa kuelekea Real Madrid hivyo haitokuwa ajabu PSG nayo ikiingia katika mbio za kuisaka saini ya Haaland.
Kimataifa Haaland kupewa mkataba mpya City
Haaland kupewa mkataba mpya City
Read also