Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema licha ya kupata ushindi Jumanne wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold lakini amekiri wapinzani wake hao walimpa wakati mgumu kutokana na malengo waliyonayo.
Mgunda alisema tangu awali alibainisha kuwa hawezi kuwadharau Geita kulingana na nafasi waliyopo ya mkiani kwenye msimamo wa ligi kwani hilo ndilo linalofanya mchezo kuwa mgumu.
Alifafanua kwamba na hicho ndicho kilichotokea katika dakika 90 za mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Alisema bado hawajamaliza kazi kwani sasa wamebakisha mechi mbili za kuwania kumaliza ligi nafasi ya pili, hivyo wanarejea kikamilifu kwenye uwanja wa mazoezi kuhakikisha wanahitimisha shughuli kwa kuchukua pointi zote sita dhidi ya KMC na JKT Tanzania.
“Kikubwa ni kwamba mechi ilikuwa ngumu na siku zote lazima tuseme ukweli, huwezi kumdharau mtu sababu ya huko aliko au matokeo yake, nilisema tangu mapema mechi itakuwa ngumu na nzito sababu kila mmoja ana malengo yake.
“Lakini yote kwa yote tunamshukuru Mungu tumepata alama tatu na mabao manne, hii imeshakwisha tunajipanga na mchezo ujao kuangalia nini cha kufanya ili tuondoke na ushindi,” alisema Mgunda.
Simba iliyopo nafasi ya tatu inapambana kumaliza nafasi ya pili ikiwa imefikisha pointi 63 sawa na Azam iliyo nafasi ya pili kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na pia imebakiwa na mechi mbili za kufunga dimba dhidi ya Kagera Sugar na Geiga Gold.
Soka Mgunda: Geita walitupa wakati mgumu
Mgunda: Geita walitupa wakati mgumu
Read also