Na Joseph Shaluwa
Staa wa burudani kutoka Tanzania, Idris Sultan (pichani) ameng’arisha ujio mpya wa tamthiliya ya Bridgerton, katika onesho kabambe lililowakusanya nyota daraja la kwanza kutoka Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla.
Onesho hilo lilifanyika mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini, ambapo Netflix, waandaaji wa series hiyo, walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton.
Msimu wa tatu wa Bridgerton unatarajiwa kurushwa na Netflix na kushuhudiwa na ulimwengu mzima ambapo tayari sehemu ya kwanza imeshaoneshwa na sehemu ya pili itaoneshwa Juni 13, mwaka huu.
Katika onesho hilo, walihudhuria mastaa wakubwa kutoka nchi za Kenya, Tanzania (Idris), Nigeria, Ghana, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini, wakiongozwa na Adjoa Andoh (ambaye amecheza kama Lady Aga kwenye Bridgerton) akiwa kama mgeni wa heshima.
Mkali wa kurapu free style, kutoka Afrika Kusini ambaye amependekezwa kwenye Tuzo za Grammy, Musa Keys naye aliungana na mastaa wenzake katika hafla hiyo.
Mbali na Idris mastaa wengine kutoka Afrika Mashariki walioalikwa katika onesho hilo la kijanja ni pamoja na komediani na mtayarishaji maudhui, Elsa Majimbo.
Wengine kutoka Kenya ni staa wa filamu Catherine Kamau (Kate), Amina Abdi Rabar na waigizaji mahiri Manasseh Nyagah na Jackie Matubia.
Wanamitindo maarufu wa Nairobi: Brian Babu na Lady Mandy pia walihudhuria, ambapo kwa pamoja walihusika katika kubuni na kutengeneza mavazi ya mastaa waliohudhuria.
Burudani Idris Sultan aing’arisha Bridgerton
Idris Sultan aing’arisha Bridgerton
Related posts
Read also