Paris, Ufaransa
Mama wa mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappé ambaye pia ndiye wakala wake, Fyza Lamari ameitaja Real Madrid timu ambayo mtoto wake anatarajia kujiunga nayo kuanzia msimu ujao.
Fayza alitoa kauli hiyo jana Jumatatu katika hafla iliyoandaliwa na Mbappe kuaga PSG ambapo mama yake alikuwa miongoni mwa wageni 250 waalikwa akiwamo rais wa Ufaransa na rais wa PSG ambao hata hivyo hawakuhudhuria.
Hafla hiyo iliyofanyika katika klabu moja ya Wataliano ya Gigi iliyopo jijini Paris, pia ilihudhuriwa na baba wa Mbappe, Wilfred, mdogo wake Ethan, ndugu wengine, marafiki pamoja na wachezaji wenzake wa PSG.
Fayza aliulizwa na waandishi wa habari ni timu gani mtoto wake anatarajia kujiunga nayo msimu ujao ambapo alijibu kwa kifupi, “Mbona wote tayari mnaijua.”
Kauli ya mama huyo imekuja wakati habari kubwa iliyopo duniani kote ni kwamba mchezaji huyo anasubiri kujiunga na Real Madrid, timu ambayo imekuwa ikiisaka saini yake tangu msimu uliopita.
Real Madrid kwa sasa inasubiri kuumana na Borussia Dortmund katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Juni Mosi kwenye dimba la Wembley na baada ya hapo ndipo itamtangaza rasmi Mbappe kuwa mchezaji wao.
Mbappe pia inadaiwa ana hamu ya kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa kwenye Michezo ya Olimpiki itakayofanyika jijini Paris lakini zipo habari kwamba mabosi wa Real Madrid wamemtaka achague kati ya Euro 2024 au Olimpiki.
Kimataifa Mama wa Mbappe aitaja Real Madrid
Mama wa Mbappe aitaja Real Madrid
Read also