Na mwandishi wetu
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta na timu yake ya PAOK wamerejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya jana Jumapili kutwaa taji la Ligi Kuu Ugiriki kwa kuifunga Aris mabao 2-1.
PAOK ambayo msimu huu ilishiriki michuano ya UEFA Europa Conference League imemaliza msimamo wa ligi hiyo ikikusanya pointi 80, mbili mbele ya AEK iliyomaliza katika nafasi ya pili.
Katika mechi hiyo, Brandon Thomas na Taison Freda waliibuka mashujaa wa PAOK wakifunga mabao mawili huku bao pekee la wenyeji, Aris katika mchezo huo likifungwa na Loren Moron.
Katika mchezo huo, Samatta alianzia benchi, lakini alingia uwanjani dakika ya 65 kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la kwanza Thomas.
Samatta licha ya kuvaa medali ya ubingwa, amepitia ukame wa muda mrefu wa kufumania nyavu ndani ya timu hiyo msimu huu huku akianzia benchi mara kwa mara na nafasi yake amekuwa akianzishwa Thomas raia wa Hispania.
Mpaka sasa Samatta aliyewahi kung’ara akiwa na TP Mazembe ya DR Congo na Genk ya Ubelgiji, amefunga mabao mawili katika Ligi Kuu Ugiriki msimu huu wakati Thomas akifumania nyavu mara saba.
Kimataifa PAOK ya Samatta kucheza Ligi ya Mabingwa
PAOK ya Samatta kucheza Ligi ya Mabingwa
Read also