Amsterdam, Uholanzi
Mshambuliaji wa zamani wa timu za Arsenal na Man United, Robin van Persie ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Heerenveen ambayo inashiriki Ligi Kuu Uholanzi maarufu Eredivisie.
Van Persie, 40, ambaye enzi zake za ushindani aling’ara zaidi akiwa Arsenal kabla ya kustaafu soka mwaka 2019, alitangazwa Ijumaa hii kubeba majukumu hayo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Kabla ya hapo, Van Persie alikuwa akifanya kazi ya ukocha katika klabu ya Feyenoord ambako ndipo alipoibukia katika kikosi cha vijana chini ya miaka 18 na kustaafia katika klabu hiyo hiyo.
Van Persie ndiye kinara wa mabao katika timu ya taifa ya Uholanzi na aliwahi kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka na kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) akiwa na Man United.
Heerenveen kwa sasa inashika nafasi ya 10 katika Eredivisie na Jumapili hii itakuwa na kibarua dhidi ya Sparta Rotterdam katika mechi ya mwisho ya msimu huu wa 2023-24.
Kimataifa Van Persie kocha mkuu Heerenveen FC
Van Persie kocha mkuu Heerenveen FC
Related posts
Read also