London, England
Matumaini ya Man City kubeba mara ya nne mfululizo taji la Ligi Kuu England (EPL) yapo juu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur ingawa kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola amesema mechi moja iliyobaki ni ngumu.
Mabao mawili ya Erling Haaland, moja kwa mkwaju wa penalti na lingine kwa pasi ya Kevin de Bruyne yalitosha kuibua matumaini hayo huku pia yakiifuta rasmi Spurs kwenye ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Na sasa Man City wanasubiri kutawazwa rasmi mabingwa wa taji hilo hapo Jumapili ila ni kama tu wataifunga West Ham katika mechi ya mwisho ya EPL msimu huu au wakifungwa waombee Arsenal nao wapoteze mechi yao ya mwisho.
Spurs hata hivyo licha ya kupoteza mechi hiyo lakini ilicheza vizuri na ilikuwa wazi kwamba matokeo mazuri ya timu hiyo si tu kwamba yangeweka hai matumaini yao ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya bali pia yangeibeba Arsenal.
Matokeo mazuri ya Spurs dhidi ya Man City yangekuwa msaada mkubwa kwa Arsenal ambao wao mechi yao ya mwisho watakuwa nyumbani Emirates dhidi ya Everton ambayo sasa si tu wanatakiwa washinde bali pia waombee Man City apoteze dhidi ya West Ham.
Arsenal imezidiwa na Man City kwa pointi moja hivyo kama Spurs ingepata ushindi dhidi ya Man City, matokeo hayo yangekuwa neema kubwa kwa Arsenal ambao japo wanafahamika kuwa mahasimu wakuu wa Spurs katika jiji la London.
Kimataifa Taji la nne EPL lanukia City
Taji la nne EPL lanukia City
Read also