Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kuwa kwa sasa hawana la kufanya zaidi ya kuwaombea mabaya walio juu yao kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Sambamba na hilo, Katwila alisema kwamba wao pia wanapambana kushinda mechi zao tatu zilizosalia ili waangukie hatua ya mechi za mtoano kupambania kusalia kwenye ligi hiyo msimu ujao.
Katwila amezungumza hayo baada ya timu yake kufungwa mabao 3-1 na Yanga na hivyo kusalia kwenye nafasi ya 16 ikiwa na pointi 20 baada ya mechi 27 walizocheza hadi sasa.
Mtibwa kwa sasa imebakiza michezo mitatu dhidi ya Namungo wakiwa nyumbani na miwili ya ugenini dhidi ya Mashujaa na Ihefu, mechi ambazo Katwila anataka wapambane kupata ushindi.
“Tunashukuru tumemaliza salama mechi ya Yanga japo lengo letu la kuchukua pointi tatu mbele ya timu bora kama Yanga halijatimia, walikuja na malengo yao pia ya kutafuta alama tatu maana wao ndiyo mabingwa watetezi.
“Kwa hiyo tulikuwa na kazi kubwa kusema kweli ya kupambana nao lakini ni bahati mbaya kwani tulitangulia baadaye wamerejsha na wakapata nguvu zaidi wakaongeza mengine.
“Lakini ilikuwa ni makosa yetu wenyewe tuliyoyafanya, wao wakatumia nafasi ingawa ukiangalia mabao yenyewe ni mepesi na unapofanya makosa kwa timu zenye kariba kama ya Yanga inakuwa tatizo.
“Kwa hiyo niwape pole wachezaji wangu kwa kufanya makosa madogo mbele ya timu bora ambapo makosa madogo yametugharimu,” alisema Katwila.
Kocha huyo wa zamani wa Ihefu, alifafanua zaidi: “Kikubwa ni kutokata tamaa sababu kama walio juu (kwenye msimamo) watatoa nafasi ya sisi kuwafikia kutokana na matokeo ya mechi zenyewe basi nafasi bado ipo na kama ikitokea tukishinda mechi zote basi tutacheza ‘play-off.
Katwila pia alikiri kuwa Mtibwa kubaki moja kwa moja kwenye ligi itakuwa ngumu kwani walio juu yao wengi washafikisha pointi za kutosha hivyo cha msingi ni kuwa makini na kushinda mechi zao na kuangalia hao wengine wamefikia wapi.
Soka Katwila aziombea dua mbaya timu pinzani
Katwila aziombea dua mbaya timu pinzani
Read also