Paris, Ufaransa
Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba yuko katika harakati za uigizaji wa filamu iliyopewa jina la 4 Zeros ambayo inatarajia kutolewa Aprili mwakani.
Pogba, nyota aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya Ufaransa kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli.
Filamu anayoigiza Pogba ni mwendelezo wa filamu ya awali y 3 Zeros ambayo ilitolewa mara ya kwanza mwaka 2002 na habari zaidi zinadai kwamba sehemu ambayo inahusika kuigiza filamu hiyo ni katika jiji la Paris.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Pogba ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31, katika filamu hiyo anaigiza kama kocha wa timu ya soka ya vijana,
Kuhusu sakata la dawa za kusisimua misuli, mchezaji huyo alisema kwamba hajawahi kutumia dawa hizo kwa makusudi na ameikatia rufaa adhabu hiyo ambayo alipewa Februari mwaka huu.
Rufaa ya Pogba itasikilizwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) na kama atafanikiwa katika rufaa hiyo huenda adhabu aliyopewa ya miaka minne ikapunguzwa.
Burudani Pogba ageukia uigizaji filamu
Pogba ageukia uigizaji filamu
Read also