Manchester, England
Klabu ya Manchester United haitarajii kupata ofa yoyote ya kumuuza mshambuliaji wake, Harry Kane ikiamini kwamba hakuna klabu ambayo itakuwa tayari kumpandia dau mshambuliaji huyo.
Katika siku za karibuni zimekuwapo habari kwamba klabu hiyo ina mpango wa kuwapiga bei baadhi ya mastaa wake huku Rashford naye akitajwa katika mpango huo lakini habari mpya ni kwamba klabu hiyo haioni sababu ya kumpunguza mshambuliaji huyo.
Man United inaamini na inatambua kwamba ni klabu ya PSG ya Ufaransa pekee inayoweza kuwasilisha ofa ya kumtaka Rashford lakini haitokuwa tayari kulipa kiwango cha mshahara wa mchezaji huyo.
Zaidi ya hilo, Man United pia inatambua kwamba japo PSG imekuwa ikimtaka mshambuliaji huyo lakini haiamini kwamba anaweza kuwa mbadala wa Kylian Mbappe ambaye zipo habari kwamba anajiandaa kujiunga na Real Madrid baada ya msimu huu.
Msimu huu umekuwa mgumu kwa Rashford akiwa hadi sasa amefunga mabao tisa tu katika mashindano yote lakini Man United haipo tayari kuona akiondoka kwa dau kupunguzwa badala yake inaona bora aendelee kubaki katika timu hiyo.
Mchezaji mwengine ambaye majaliwa yake Man United hayajawekwa sawa ni Mason Greenwood ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Getafe ya Hispania akiwa akiwa katika msimu wake wa kwanza na tayari ameifungia mabao 10.
Greenwood, 22, ambaye alikuwa akiandamwa na kesi ya udhalilishaji ambayo hata hivyo ilifutwa Februari mwaka jana kwa kukosekana ushahidi na baadhi ya mashahidi kujitoa, huenda naye akauzwa jumla au kurudishwa kikosini.
Kimataifa Man Utd haitarajii kumuuza Rashford
Man Utd haitarajii kumuuza Rashford
Read also