Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema amefurahishwa kurejea kwenye uwanja mzuri na rafiki kuelekea mechi yao ya kesho Jumamosi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Coastal Union mechi itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Gamondi raia wa Argentina, ameyasema hayo baada ya kupata suluhu dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wao wa mwisho wa ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo.
Kocha huyo alisema kwamba uwanja huo haukuwa rafiki kutokana na kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini na hivyo kuvuruga mipango yao mingi ya ushindi.
“Tumetoka kucheza mchezo wa kwenye mazingira magumu na tuna njaa ya kupata alama tatu. Hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu Coastal ni wazuri kwenye kuzuia mashambulizi, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho,” alisema Gamondi.
“Mechi zinapokuwa karibu sana muda wa maandalizi unakuwa mdogo, jana tumefanya mazoezi ya kurejesha miili sawa kwa wachezaji na leo (Ijumaa) tutapata muda kidogo wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho na hapo ndipo nitajua wachezaji wa kuwatumia,” alisema Gamondi.
Mchezo wa kesho unahitaji sana ubora wa wachezaji na angalau tunaenda kucheza kwenye uwanja wenye mazingira mazuri, muhimu zaidi kesho ni kuweka mpira wavuni na kuibuka na ushindi,” alisema Gamondi.
Yanga ambayo inaongoza ligi kwa pointi 59 baada ya mechi 23, itaivaa Coastal iliyo kwenye nafasi ya nne na pointi zao 33 baada ya kushuka dimbani mara 23.
LigiKuu Gamondi afurahia uwanja mzuri
Gamondi afurahia uwanja mzuri
Read also