Na mwandishi wetu
Yanga wameendelea kushangilia ushindi wao wa Jumamosi iliyopita dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC kwa kuweka mabango ya matangazo makubwa jijini Dar es Salaam kuhusu matokeo ya mchezo huo.
Timu hiyo hata hivyo imekwenda mbali zaidi katika matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwani wameweka mabango hayo leo Jumanne sehemu mbalimbali.
Mabango hayo ambayo ni dhahiri yamewekwa kwa ajili ya kuwakera mahasimu wao Simba, yanasomeka Yanga 7 Simba 2 licha ya kuwa mchezo huo uliisha kwa Yanga kushinda mabao 2-1.
Yanga imefanya hivyo ikijumlisha matokeo ya jumla pamoja na ya mechi yao ya awali ya Ligi Kuu NBC walipowafunga Wekundu hao mabao 5-1 na hivyo kuandika rekodi ya kuchukua pointi sita dhidi ya mahasimu wao hao ndani ya msimu mmoja.
Yanga inayopambana kutetea ubingwa wa ligi ikiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 58 baada ya mechi 22 na kuiacha Simba inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi 46 kwa mechi 21, iliwahi kuweka mabango hayo pia walipoitungua Simba mabao 5-1.
Soka Yanga yatumia mabango kuinanga Simba
Yanga yatumia mabango kuinanga Simba
Read also