Madrid, Hispania
Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham ametwaa tuzo ya Laureus World Sports kwa namna alivyopata mafanikio akiwa katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo na kuwa moto kwenye ligi mpya kwake.
Bellingham alijiunga na Real Madrid majira ya kiangazi msimu huu kwa ada ya Pauni 89 milioni akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani na tangu wakati huo ameendelea kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo.
Juzi Jumapili, Bellingham alifunga bao la ushindi dhidi ya Barcelona katika El Clasico na hadi sasa ana mabao 17 katika Ligi Kuu Hispania au La Liga.
Bellingham pia ameiwezesha Real Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuwatoa mabingwa watetezi Man City kwa mikwaju ya penalti kwenye hatua ya robo fainali.
Kwa upande mwingine tuzo kuu ya mwaka ya Laureus World Sports imekwenda kwa nyota wa tenisi Novak Djokovic ambaye anakuwa ameibeba tuzo hiyo kwa mara ya tano.
Tuzo aliyotwaa Djokovic kwa upande wa wanawake imekwenda kwa kiungo wa timu ya wanawake ya Barcelona ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Aitana Bonmati.
Bonmati ambaye kwa sasa anashikilia tuzo ya Ballon d’Or ameisaidia klabu yake kushinda mataji ya Liga F, Spanish Cup na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wanawake msimu wa 2022-23.
Katika vipengele vingine vya tuzo hiyo, timu ya wanawake Hispania imetwaa tuzo ya timu ya mwaka wakati nyota wa tenisi Hispania, Diede de Groot amebeba tuzo ya mwaka kwa upande wa wanamichezo wenye ulemavu.
,
Kimataifa Bellingham atwaa tuzo Hispania
Bellingham atwaa tuzo Hispania
Read also