London, England
Rufaa ya Everton kupinga kupokwa pointi kwa kosa la kwenda kinyume na kanuni za Ligi Kuu England za matumizi ya fedha, itasiklizwa haraka na uamuzi kutolewa kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi.
Awali Everton ilipokwa pointi 10 na baadaye adhabu kubadilishwa na kuwa pointi sita baada ya kukata rufaa Februari mwaka huu kwa kosa ambalo wanadaiwa kulifanya kwa miaka mitatu hadi kufikia msimu wa 2021-2022.
Taarifa ya wasimamizi wa Ligi Kuu England ilieleza kuwa klabu ya Everton ilikata rufaa Jumatatu (jana) na rufaa hiyo itasikilizwa haraka.
Everton inayonolewa na kocha Sean Dyche kwa sasa inashika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi mbili zaidi ambazo zinaitoa kwenye hofu ya janga la kushuka daraja.
Kanuni ambayo Everton inadaiwa kuivunja inahusu faida endelevu ambapo klabu zinaruhusiwa kupoteza au kupata hasara isiyozidi Pauni 105 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu lakini Everton inadaiwa kuzidisha kiasi hicho kwa Pauni 16.6 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu hadi msimu wa 2022-2023.
Hata hivyo kuna hofu kwamba suala hilo huenda likachukua muda kufikia hitimisho hadi baada ya msimu huu wa Ligi Kuu England.
Mechi za mwisho za Ligi Kuu England zinatarajia kuchezwa Mei 19 na tayari wajumbe wa bodi watakaosikiliza rufaa hiyo wameshatangazwa.
Kimataifa Everton wakomalia pointi 6 walizopokwa
Everton wakomalia pointi 6 walizopokwa
Read also