Madrid, Hispania
Uongozi wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ unadaiwa kuachana na uchunguzi kuhusu malalamiko ya klabu ya Getafe dhidi ya kauli anazodaiwa kutolewa mchezaji wao Mason Greenwood na Jude Bellingham wa Real Madrid.
Nyota hao wote wa England inadaiwa waliingia katika utata na kutoleana kauli zisizopendeza wakati wa mechi baina ya timu zao iliyopigwa Februari Mosi ambapo Bellingham anadaiwa kutoa kauli zenye utata kwa Greenwood.
Katika mechi hiyo ambayo iliisha kwa Real Madrid kutokana na ushindi wa mabao 2-0, Bellingham anadaiwa kumtolea Greenwood kauli zisizofaa wakati wachezaji hao wakiwania mpira na tukio hilo kuwa mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

Habari zaidi zinadai kwamba maofisi wa La Liga waliomba msaada wa wataalam wa ‘kusoma midomo’ ili kujua msemaji alisema nini lakini uchunguzi wa sakata hilo haujakamilika huku kukiwa na habari kwamba umemalizwa kimya kimya.
Bellingham ambaye ndiye aliyemkaba Greenwood katika tukio na ndiye mtuhumiwa lakini zipo habari za vyanzo mbalimbali pia zinazodai kwamba Greenwood ameomba uchunguzi wa tukio hilo uachwe.