Na mwandishi wetu
Timu ya Taifa ya riadha ya mbio za Nyika imeshindwa kwenda Belgrade, Serbia kushiriki mashindano ya Dunia yatakayoanza leo Ijumaa baada ya baadhi ya wachezaji kukosa visa.
Timu hiyo yenye wachezaji tisa, ambayo ilikuwa kambini Ngaramtoni, Arusha kuanzia Machi 22, mwaka huu ilitarajiwa kuondoka juzi Machi 27, mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na changamoto hiyo.
Wachezaji waliotarajiwa kusafiri kwa wanaume ni Herman Sulle, Boay Dawi, Dectaforce Boniface, Mao Ako na John Nahhay na wanawake ni Hamida Nassoro, Neema Festo, Ernestina Mngolale na Anastazia Dolomongo na kocha Marcelina Gwandu.
Akizungumza leo Ijumaa, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Silas Isangi (pichani) alikiri kuhusiana na hilo: “Wanariadha walitarajiwa kuondoka tarehe 27 lakini ililazimika kusogeza mbele safari yao hadi tarehe 28 baada ya kuchelewa kupata viza kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Alisema maombi ya viza yalifanyika Machi 8, mwaka huu kwenye ubalozi wa Serbia uliopo Nairobi nchini Kenya lakini mpaka Machi 27 ni wachezaji watano tu waliofanikiwa kukamilisha upatikanaji wa nyaraka hizo.
Alisema ndege ya KLM inatarajia kuondoka kesho Jumamosi saa nne asubuhi, kutoka Tanzania kupitia Entebbe, Uganda hivyo wangechelewa kufika Amsterdam, Uholanzi kwa ajili ya kuunganisha kwenda Serbia.
Riadha Viza zawakosesha mashindano wanariadha
Viza zawakosesha mashindano wanariadha
Read also