London, England
Mshambuliaji wa zamani wa timu za Liverpool na Tottenham Hotspur, Peter Crouch amemtaja beki wa zamani wa Chelsea, John Terry kuwa ndiye beki mpambanaji na aliyempa tabu kati ya wote aliowahi kukutana nao katika soka la ushindani.
Crouch (pichan) ambaye pia amewahi kuichezea timu ya taifa ya England na klabu kadhaa, amewahi kukutana na mabeki wengi enzi zake kabla ya kustaafu soka lakini amekiri kwamba alikuwa akipata tabu kwa Terry.
“Nakumbuka pia nikiwa QPR, ilikuwa mechi ya kikombe si ya Ligi Kuu England, kulikuwa na Tony Adams na nafikiri pia alikuwapo Steve Bould,” alisema Crouch akiwataja mabeki wengine.
“Pia nafikiri kwa miaka kadha amekuwapo Sol Campbell, naye alinipa majaribu kwa sababu ana mwili na ni mwenye miguvu,” aliongeza Croch.
Crouch hata hivyo alisema kwamba anadhani John Terry ndiye aliyekuwa bora kati ya mabeki wote aliowahi kukutana nao enzi zake za soka la ushindani.
Kimataifa Peter Crouch amkumbuka John Terry
Peter Crouch amkumbuka John Terry
Related posts
Read also