Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Geita Gold FC, Denis Kitambi amesema atazitumia mechi tisa zilizobaki kuiweka timu hiyo sehemu salama kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Kitambi alisema hiyo ni kutokana na kutumia mapumziko ya wiki mbili ya ligi kuimarisha upungufu wa kikosi chake uliosababisha kupoteza mechi kadhaa.
“Mechi zote tisa zilizobaki tumezipa hadhi ya fainali, malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ili kujiondoa kwenye nafasi mbaya tuliyopo hivi sasa na hilo linawezekana sababu kitu kizuri ni kwamba mechi zote dhidi ya timu kubwa tumeshamalizana nazo,” alisema.
Alisema kinachompa matumaini na uhakika wa kushinda mechi hizo ni kuimarika kwa kikosi chake baada ya kurekebisha makosa madogo madogo ambayo yalikuwa yakijirudia mara kwa mara kabla ya ligi haijasimama.
Pia alisema kila mchezaji amempangia jukumu lake la kufanya katika kila mechi watakayocheza na masharti yake ni kuhakikisha anatimiza kwa asilimia 75 kwenda juu akiamini hiyo ni moja ya mbinu itakayowasaidia kupata ushindi.
Geita ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa imevuna pointi 21 katika idadi kama hiyo ya mechi na Kitambi amesema hayupo tayari kuona timu hiyo inashuka daraja.
Soka Kitambi ataja mechi 9 za kumpaisha
Kitambi ataja mechi 9 za kumpaisha
Related posts
Read also