Manchester, England
Bilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Man United, Sir Jim Ratcliffe inadaiwa amemtaja kocha wa England, Gareth Southgate kuwa chaguo la kwanza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag katika timu hiyo.
Mpango wa kumchukua Southgate unatajwa kuwa ni mojawapo ya mikakati ya bilionea huyo yenye lengo la kuibadili timu hiyo jambo ambalo aliahidi kulifanya tangu anunue hisa.
Mambo mengine ambayo bilionea huyo ana mpango wa kuyafanya ni pamoja na kuboresha uwanja unaomilikiwa na klabu hiyo wa Old Trafford licha ya upinzani uliojitokeza.
Wiki kadhaa zilizopita mpango wa bilionea huyo kumtaka Southgate uliibuka na kupata nguvu kutokana na matokeo mabaya ya Man United na sasa umeibuka kwa mara nyingine licha ya timu hiyo kuanza kupata mafanikio katika mechi za hivi karibuni.
Bilionea huyo hata hivyo inadaiwa ameshikilia mpango wa kumtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 ili ajiunge na timu hiyo wakati wa majira ya kiangazi na anataka uamuzi wa jambo hilo ufikiwe haraka.
Swali linabaki kwa Southgate, je atakuwa tayari kuachana na timu ya England ili apate nafasi ya kuinoa Man United licha ya ukweli kwamba England imeonekana kuwa bora chini yake na bado anahitajika.
Kimataifa Bilionea Man United amtaka Southgate
Bilionea Man United amtaka Southgate
Read also