Na mwandishi wetu
Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema chini ya kocha Abdelhak Benchikha anaamini wataifunga Al Ahly na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya Simba na Al Ahly umepangwa kuchezwa Machi 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam kabla ya kurudiana baada ya wiki mbili.
“Ni kweli Al Ahly ni timu kubwa na ina uzoefu mkubwa kwenye hatua hizi lakini Simba tuna kocha mkubwa anayewajua vyema wapinzani, naamini mbinu zake na kujituma kwetu ndio mafanikio,” alisema Tshabalala.
Alisema wanawajua vyema wapinzani wao sababu wameshakutana nao kwenye michuano ya AFL na kutoka sare katika mechi zote mbili hivyo wanapo pa kuanzia.
Simba imepangwa na Al Ahly baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye mechi za hatua ya makundi ya michuano hiyo na safari hii imedhamiria kufika hatua ya nusu fainali.
Soka Zimbwe Jr apiga hesabu za nusu fainali Afrika
Zimbwe Jr apiga hesabu za nusu fainali Afrika
Read also