Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite Queens imeaga Michezo ya Afrika licha kutoka sare ya bao 1-1 na Ethiopia katika michezo hiyo inayoendelea Accra, Ghana.
Tanzanite Queens imeaga mashindano hayo ikiwa na pointi mbili na Ethiopia pointi moja huku wenyeji Ghana na Uganda wakisonga mbele wakiungana na Nigeria na Senegal katika nusu fainali.
Katika mashindano hayo yatakayofikia tamati Machi 23, mwaka huu, Tanzanite ilipata matokeo mengine ya sare dhidi ya Uganda kabla ya kufungwa na wenyeji Ghana mabao 2-1.
Nusu fainali, Ghana itacheza na Senegal na Nigeria itaumana na Uganda. Michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumatatu.
Ukiachilia soka pia kwenye michezo mingine ambayo Tanzania imeaga ni baiskeli, judo, kriketi wanaume na wanawake na kuogelea na sasa zimebaki timu za ngumi na riadha ambao wataanza kukimbia keshokutwa.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 53 zinazoshiriki michezo hiyo inayoshirikisha wanamichezo 2,644 na mpaka sasa haijapata medali yoyote.
Kimataifa Tanzanite yaaga Michezo ya Afrika
Tanzanite yaaga Michezo ya Afrika
Read also