London, England
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Man City wamepangwa kucheza na Real Madrid katika hatua ya robo fainali ya ligi hiyo wakati Arsenal wakipangwa kuumana na Bayern Munich.
Katika mechi ya kwanza ya ligi hiyo, Arsenal ndio watakaokuwa nyumbani wakiikaribisha Bayern ambayo itakuwa na nahodha wa England na mchezaji wa zamani wa Tottenham, Harry Kane katika safu yao ya ushambuliaji.
Kwa Man City ugumu wa hatua hiyo utaanzia katika mtihani wake na mabingwa hao mara 14 wa michuano hiyo ambayo mechi za kwanza za robo fainali zitapigwa Aprili 9 na 10 na marudiano Aprili 16 na 17.
Katika droo hiyo timu hizo za England zote zitaanza mechi zao Aprili 9, wakati Arsenal ikiwa nyumbani Emirates, City wao watakuwa wageni wa Real Madrid kwenye dimba la Bernabeu.
Na kama itatokea kwa Man City kuibwaga Real Madrid na Arsenal kuibwaga Bayern, timu hizo za England zitacheza zenyewe katika hatua ya nusu fainali kusaka tiketi ya fainali.
Kwa mujibu wa droo hiyo, mechi nyingine za hatua hiyo zitawakutanisha PSG watakaoumana na Barcelona wakati Atletico Madrid wataonyeshana kazi na Borussia Dortmund.
Mechi za nusu fainali zitapigwa kati ya Aprili 30 na Mei Mosi na marudiano wiki moja baadaye wakati mechi ya fainali itapigwa Juni Mosi kwenye dimba la Wembley.
Ratiba kamili ya mechi za robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama ifuatavyo…
Arsenal v Bayern Munich
Atletico Madrid v B. Dortmund
PSG v Barcelona
Real Madrid v Man City
Kimataifa Man City yapewa Real Madrid robo fainali Ulaya
Man City yapewa Real Madrid robo fainali Ulaya
Read also