Na mwandishi wetu
Kipa wa Coastal Union, Ley Matampi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu NBC huku kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, akiibuka kocha bora wa mwezi huo.
Matampi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa kucheza dakika 270 za michezo mitatu bila kuruhusu bao mwezi Februari, ambapo aliisaidia Coastal Union kushinda bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, kisha kuichapa bao 1-0 Mtibwa Sugar na kulazimishwa sare ya bila kufungana na KMC.
Matampi amewashinda Mudathir Yahya wa Yanga na Samson Mbangula na Prisons alioingia nao fainali huku akiwa ameisaidia Coastal kupanda kutoka nafasi ya sita hadi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Upande wa Gamondi mwezi Februari aliiongoza Yanga katika michezo mitano ikishinda minne na kutoka sare mara moja.
Kocha huyo aliiongoza Yanga katika suluhu dhidi ya Kagera Sugar, ikaichapa Dodoma Jiji 1-0 kisha, ikaifunga Mashujaa mabao 2-1, wakashinda 2-1 mbele ya Prisons na wakaicharaza KMC mabao 3-0.
Gamondi alishinda tuzo hiyo akiwashinda Abdelhak Benchikha wa Simba na Hamad Ally wa Prisons ambao aliingia nao fainali.
Soka Gamondi, Matampi wang’ara Februari
Gamondi, Matampi wang’ara Februari
Read also