Na mwandishi wetu
Kocha wa muda timu ya Singida Fountain Gate, Ngawina Ngawina amesema lengo lake ni kuhakikisha timu hiyo inarudi kwenye ushindani wa kuwania taji la Ligi Kuu NBC kwa kupata matokeo mazuri.
Ngawina ameyasema hayo Ijumaa hii akieleza timu hiyo imejiweka katika daraja la timu zinazoshiriki mashindano ya kimataifa kutokana na aina ya wachezaji inayowasajili na uendeshwaji wake kwa hiyo ni lazima wapambane ili kuipata nafasi hiyo mwishoni mwa msimu.
“Kazi yangu ni kuhakikisha ushindi katika mechi zilizo mbele yetu na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, najua si kazi rahisi kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi tofauti na Championship lakini lazima tupambane,” alisema Ngawina.
Kocha huyo aliyewahi kuichezea TP Mazembe ya DR Congo, alisema anajivunia ubora wa kikosi chake chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kupambana kutimiza malengo kwa hiyo yupo tayari kuhakikisha kazi aliyopewa anaitimiza.
Ngawina anashirikiana na kocha wa makipa, Ally Mustapha ‘Barthez’ kuinoa timu hiyo iliyopo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21.
Hivi karibuni uongozi wa Singida FG ulivunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa chini ya Thabo Senong kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo mfululizo.
Soka Ngawina kuirudisha Singida kwenye ushindani
Ngawina kuirudisha Singida kwenye ushindani
Read also