Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Francis Baraza ameomba wiki mbili zaidi ili kikosi chake kipate muunganiko na kucheza soka la kuvutia.
Akifafanua kuhusu hilo, Baraza alisema matokeo ya kusuasua wanayoyapata kwenye mechi za ligi yanatokana na falsafa mpya alizoziingiza tangu akabidhiwe timu hiyo hivi karibuni akichukua mikoba ya Melis Medo aliyejiweka pembeni.
“Kwanza nawashukuru mashabiki kwa uvumilivu lisha ya kutokuwa na matokeo ya kuridhisha lakini nawaomba wanipatie wiki mbili kila kitu kitakuwa sawa sababu tupo katika kipindi cha kutengeneza timu na wakati huo huo tunahitaji matokeo, si rahisi kupata vyote kwa pamoja,” alisema Baraza.
Kocha huyo alisema mpango wake ni kuiona timu hiyo inacheza soka la kuvutia na kushinda bila kutumia nguvu kama alivyofanya akiwa na timu za Biashara United na Kagera Sugar.
Alisema hilo linawezekana kutokea Dom Jiji lakini inahitaji muda ndio maana ameomba wiki mbili na baada ya hapo atafanya usajili kwenye dirisha kubwa ambalo litaifanya timu hiyo kuwa ya kuogopwa na wapinzani.
Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United hivi majuzi, umeipandisha timu hiyo hadi nafasi ya tisa ikikusanya pointi 23 katika michezo 19 iliyocheza hadi sasa.
Soka Baraza aomba wiki mbili Dom Jiji
Baraza aomba wiki mbili Dom Jiji
Read also