Na mwandishi wetu
Wachezaji wa Yanga; Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua na Nickson Kibabage wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Februari wa timu hiyo.
Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema Jumatatu hii sababu ya kupendekezwa wachezaji hao ni kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwa timu yao mwezi uliopita.
“Hao ndio wachezaji ambao rekodi zao zimeonesha kuibeba sana Yanga, wamefunga mabao na kutengeneza nafasi kwenye mashindano yote ndio maana tukawapendekeza kuwania tuzo hiyo ya NIC (Shirika la Bima la Taifa),” alisema Walter.
Meneja huyo alisema kazi inabaki kwa mashabiki wao kupiga kura kupitia mtandao wa klabu hiyo kuchagua mchezaji ambaye wanaamini ndiye bora ili awe mshindi wa tuzo hiyo.
Hiyo ni mara ya pili kwa Pacome kuingia kwenye kuwania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi wa Yanga. Mara ya kwanza ilikuwa Novemba, mwaka jana ambapo aliibuka mshindi dhidi ya Dickson Job na Clement Mzize.
Soka Kibabage, Pacome, Mudathir wawania tuzo Yanga
Kibabage, Pacome, Mudathir wawania tuzo Yanga
Read also