Valencia, Hispania
Kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham amelimwa kadi nyekundu baada ya kumlalamikia mwamuzi kwa kumnyima bao ambalo lingeiwezesha timu yake kutoka na ushindi wa mabao 3-2 badala yake timu hiyo iliambulia sare ya 2-2 dhidi ya Valencia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi jioni, Real Madrid ililazimika kupambana kusaka mabao ya kusawazisha baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Duro dakika ya 27 na Yaremchuk dakika ya 30.
Real Madrid waliokolewa na mabao mawili ya dakika za 45 za 76 yaliyofungwa na Vinicius Jr ambaye katika hali ya kushangaza inadaiwa alijikuta akikumbana na kadhia ya ubaguzi wa rangi, tukio ambalo pia alikutana nalo msimu uliopita.
Katika dakika ya sita muda wa nyongeza, Belllingham aliujaza mpira wavuni kwa kichwa lakini mwamuzi Gil Manzano alipuliza filimbi kuashiria kumalizika kwa mchezo kabla krosi iliyozaa bao hilo haijapigwa.
Matokeo hayo yameendelea kuiimarisha Real Madrid kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi saba lakini tukio hilo lilimkera Bellingham ambaye alijikuta akiingia katika mzozo na mwamuzi huyo.
Wachezaji na maofisa wa Real Madrid walianza kumzonga Manzano na katika tukio hilo mwamuzi huyo alimpa Bellingham kadi nyekundu kwa kinachodhaniwa kuwa ni ushiriki wake katika mzozo huo.
Kimataifa Bellingham alimwa kadi nyekundu
Bellingham alimwa kadi nyekundu
Read also