Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa maboresho waliyoyafanya kwenye dirisha dogo ambayo yamebadilisha mwenendo wa kikosi hicho.
Kocha huyo alisema siri ya timu hiyo kufanya vizuri tangu kuanza kwa mzunguko wa pili ni ubora wa maingizo mapya kwenye usajili wa dirisha dogo.
“Naupongeza uongozi kwa kunisikiliza na kutekeleza kile nilichowaomba, kwa namna tulivyo sasa tunaweza kupambana na timu yoyote na kupata matokeo mazuri bila shaka,” alisema Baresi.
Kocha huyo alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza kulitokana na kukosa wachezaji wenye uzoefu wa ligi hiyo lakini maingizo waliyofanya kwenye dirisha dogo yameziba madhaifu yaliyokuwepo.
Alisema baada ya kutoka nafasi ya 15 waliyokuwepo kwa muda mrefu mikakati yao kwa sasa ni kuendelea kupambana ili kupata matokeo mazuri yatakayowapandisha kwenye nafasi za katikati ya msimamo wa ligi.
Mashujaa juzi iliizamisha Namungo bao 1-0 na kupanda hadi nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 18 katika michezo 19 iliyocheza.
Soka Baresi aupa tano uongozi Mashujaa
Baresi aupa tano uongozi Mashujaa
Read also