Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma, (pichani) amesema mchezo wao dhidi ya Tabora United utakuwa mgumu lakini anakiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanapata ushindi.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
“Ni mchezo mgumu ukizingatia tutakuwa ugenini lakini malengo yetu ni ushindi na tutahakikisha tunacheza kwa juhudi kuhakikisha hatupotezi mchezo huu, ni mchezo muhimu, kila mmoja anajiandaa vya kutosha,” alisema Ouma raia wa Kenya.
Kocha huyo alisema wanataka kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao hivyo ni lazima wapambane ili kubaki kwenye nafasi za juu za kushiriki michuano hiyo mwisho wa msimu.
Wagosi wa Kaya hao wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakikusanya pointi 26 katika michezo 17 waliyocheza hadi sasa.
Soka Ouma akiri mechi na Tabora ngumu
Ouma akiri mechi na Tabora ngumu
Read also