London, England
Adhabu iliyopewa klabu ya Everton ya kupokwa pointi katika Ligi Kuu England (EPL) kwa kosa la kwenda kinyume na kanuni ya matumizi ya fedha, imepunguzwa kutoka pointi 10 za awali hadi sita.
Hatua hiyo imekuja baada ya Everton kuikatia rufaa adhabu ya awali ya kupokwa pointi 10 iliyotolewa Novemba mwaka jana baada ya klabu hiyo kudaiwa kukiuka kanuni inayohusu faida na ustawi wa klabu au PSR kwa kipindi cha miaka mitatu hadi msimu wa 2021-22.
Adhabu hiyo ambayo ni kubwa katika historia ya EPL iliishusha Everton katika msimamo wa ligi hiyo kutoka nafasi ya 14 hadi ya 19 na baada ya kupunguziwa adhabu sasa timu hiyo inapanda kutoka nafasi ya 17 hadi 15.
Everton hata hivyo huenda ikajikuta katika majanga mengine baada ya kushitakiwa mwezi uliopita kwa mara ya pili ikidaiwa kwenda kinyume na kanuni kwa mara nyingine katika misimu mitatu hadi msimu wa 2022-23 na kesi hiyo inatarajia kusikilizwa Aprili 8.
Baada ya kupunguziwa adhabu klabu ya Everton imedai kuridhishwa na uamuzi huo uliotolewa na bodi iliyosikiliza rufaa ya klabu hiyo na ipo tayari kushiriki kikamilifu katika kesi ya pili.
Kupunguzwa kwa adhabu hiyo kunaifanya Everton iwe imejiweka mbali kidogo na janga la kushuka daraja kwa tofauti ya pointi tano bado inalazimika kupambana katika mechi 12 zilizobaki kabla ya msimu huu wa ligi kufikia tamati.
Kimataifa Everton yapunguziwa adhabu EPL
Everton yapunguziwa adhabu EPL
Read also