Na mwandishi wetu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), imeuahirisha mchezo wa Ligi Kuu NBCkati ya Simba SC na Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa Februari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sababu iliyotajwa ya kuahirisha mchezo huo katika taarifa ya bodi iliyotolewa leo Ijumaa ni kutoa mafasi zaidi ya maandalizi na taratibu za safari kwa Simba kuelekea mchezo wake wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba inajiandaa kuumana na Asec Mimosas ya Ivory Coast, mchezo unaotarajiwa kupigwa Februari, 23 mwaka huu.
Mchezo huo ni muhimu kwa Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Kundi B ikiwa na pointi tano nyuma ya Asec Mimosas wanaoongoza wakiwa na pointi 10.
Timu ya Jwaneng Galaxy iko nafasi ya tatu kwa pointi nne na Wydad AC inaburuza mkia kwa pointi tatu baada ya kila timu kucheza mechi nne.
Simba watakuwa wageni wa mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Le Felicia mjini, Abidjan kuanzia saa 4.00 usiku huku kukiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1, timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa awali Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Soka Mechi ya Simba, Mtibwa yaahirishwa
Mechi ya Simba, Mtibwa yaahirishwa
Read also