Na mwandishi wetu
Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema kwa sasa amepona kabisa maumivu ya goti na yupo tayari kuipigania timu yake katika michuano yote inayoshiriki.
Kipa huyo alisema Jumatano hii kuwa kwa sasa anafanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa lengo la kurejea kwenye kiwango chake ili kuipigania timu yake.
“Kwa sasa nimepona, sihisi tena yale maumivu ambayo nilikuwa nikihisi wakati naanza mazoezi mepesi lakini hata madaktari wamenipa ruhusa, kitu cha msingi kwa sasa ni kupigania nafasi yangu kufikia malengo tuliyokusudia kuyafikia msimu huu,” alisema Manula.
Alisema pamoja na kukaa nje muda mrefu bila kucheza lakini anajivunia uzoefu alionao, kitu ambacho kilimsaidia kucheza mechi zote tatu akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon iliyomalizika majuzi nchini Ivory Coast.
Manula alikaa nje kwa kipindi cha miezi sita akiuguza goti alilofanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita dhidi ya Ihefu.
Kipa huyo alirejea uwanjani Novemba 5, mwaka jana na kukumbana na kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa watani zao wa jadi, Yanga katika mechi ya Ligi Kuu NBC.
Soka Manula: Niko fiti kuipigania Simba
Manula: Niko fiti kuipigania Simba
Read also