Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera amesema amewaona wapinzani wao Tabora United si timu ya kubeza, wana kikosi kizuri kinachocheza kitimu hivyo wanapaswa kufanya kazi ya ziada ili kuondoka na ushindi.
Namungo wanashuka kwenye mechi hiyo kesho Jumapili kwenye, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora wakiwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa pointi 17, wamecheza mechi 14, wakishinda mechi nne, sare tano na kupoteza mitano.
Zahera alisema Ijumaa hii kuwa amefurahi kuona vijana wake wameupa uzito mchezo huo ambao utakuwa wa kwanza kwao tangu mwaka 2024 uanze.
“Hiyo yote ni kwa ajili ya kujitayarisha na mchezo wa Tabora United, inaonesha kuna kitu kimewagusa kwenye mioyo yao na wanaelewa kuwa wao ndio watendaji wa mwisho .
“Ukikubali kuvaa gwanda wewe ni mwanajeshi vijana baada ya kuzungumza wanaelewa nini Namungo wanataka kutoka kwao, naamini watajitoa kwa ajili ya mchezo huo ambao si mwepesi hata kidogo kutokana na ubora wa Tabora,” alisisitiza Zahera.
Soka Zahera aipigia hesabu Tabora Utd
Zahera aipigia hesabu Tabora Utd
Read also